Home Sports FEI TOTO: BADO NINA NAFASI YA KUFANYA VIZURI YANGA

FEI TOTO: BADO NINA NAFASI YA KUFANYA VIZURI YANGA

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amefunguka kuwa bado anaiona nafasi yake katika kikosi cha timu hiyo kutokana na malengo aliyojiwekea kwamba anahitaji kufanya vizuri zaidi ya sasa ikiwa ni msimu mpya wa 2021/22 umeanza kwa kasi kubwa.

Fei Toto anayefundishwa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ameanza msimu huu vizuri huku akiwa kinara wa mabao kwenye kikosi hicho ndani ya Ligi Kuu Bara akifunga mawili ambapo aliwatungua Kagera Sugar na KMC ilikuwa ni mwendo wa mojamoja.

Fei Toto amesema: “Kila mchezaji anahitaji kuwa na nafasi kubwa ya kuanza katika timu, hivyo kwa upande wangu naiona nafasi yangu katika kikosi cha Kocha Nabi (Nasreddine) kwani nahitaji kufanya vizuri zaidi.

“Mipango yangu msimu huu ni kuhakikisha nafunga mabao mengi ili kuwa kinara wa mabao na kuipatia timu yangu ubingwa,”.

Yanga inasaka ubingwa ulio mikononi mwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ambaye yupo kwa muda baada ya Didier Gomes kuchimbishwa baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa Uwanja wa Mkapa mabao 3-1.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Botswana Simba ilishinda mabao 2-0 ngoma ikapinduka Uwanja wa Mkapa ikiwa ni kipigo kikubwa kwa Simba ikiwa nyumbani kwenye mechi za kimataifa baada ya kuyeyuka miaka 8 bila kufungwa katika uwanja huo.

Previous articleMOUNT ACHEKELEA KUWATUNGUA NORWICH
Next articleAZAM FC WAPEWA ONYO NA TFF