Home Sports SIMBA YAPANGWA NA RED ARROWS MTOANO SHIRIKISHO AFRIKA

SIMBA YAPANGWA NA RED ARROWS MTOANO SHIRIKISHO AFRIKA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Simba wana kazi ya kupambana mbele ya Red Arrows FC katika mchezo wa kwanza ambapo watakuwa nyumbani.

Baada ya Simba kufungashiwa virago katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy, Uwanja wa Mkapa sasa kazi yao ni kwenye Kombe la Shirikisho.

Itakuwa ni Novemba 28 ambapo Simba inatarajiwa kuchezwa na Red Arrows Uwanja wa Mkapa Novemba 28 kisha kazi ya pili itakuwa ugenini Desemba 5 nchini Zambia.

Kwa mujibu wa Didier Gomes aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa anaona timu hiyo inakwenda kufanya vizuri kwenye mashindano hayo makubwa.

Previous articleHAJI MANARA:TUMEJIPANGA KUSHINDA MBELE YA AZAM
Next articleKOCHA MPYA SIMBA APEWA SAA 48,GOMES AITAJA YANGA