Home Sports GOMES AFUNGUKA KILICHOMUONDOA SIMBA – VIDEO

GOMES AFUNGUKA KILICHOMUONDOA SIMBA – VIDEO

ALIYEKUWA kocha mkuu wa Simba, Didie Gomes amesema ameomba kujiondoa kwenye klabu hiyo baada ya kushinfwa kufikia malengo kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

“Ninapenda kuwa muwazi kwa mashabiki na wapenzi wa mpira nchini Tanzania, nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ukocha Mkuu wa Simba Sc kwa sababu ninaamini ndiyo maamuzi sahihi kwa manufaa ya klabu.”

“Baada ya mechi ile tulikuwa kwenye wakati mgumu, disappointment ni kubwa sana, huzuni ni kubwa, mimi kama kocha mkuu nina wajibu wa kuwajibika kwenye hili, ndiyo maana nikachukua maamuzi ya kujiuzulu.”

 

“Ninawashukuru sana mashabiki wa Simba kwa sapoti yao, wamekuwa na mimi kila siku. Ninamshukuru kocha wangu msaidizi, tumefanya kazi kubwa katika kipindi chote ambacho tumekuwa wote Simba, kocha wangu wa makipa naye amefanya kazi kubwa sana.”

 

“Mwanzo wa msimu tumeanza na wachezaji wengi wapya, wachezaji wetu wawili wameondoka (Miquissone na Chama), ni jambo gumu kidogo. Lakini kama ambavyo nimekuwa nikisema, kwa kikosi hiki cha Simba, kinaweza kufanya makubwa na kufika mbali.”

 

“Kilichotokea binafsi kimenihuzunisha na kimeweka doa kwenye carrier yangu ya ukocha, ni wakati wa kujipanga na kufanya makubwa zaidi. Kwa upande wa Simba ninaamini wakijipanga vizuri watashinda Ligi na Shirikisho.”

 

“Kwanza namshukuru Mo Dewji kwa sababu ni mtu wa kutekeleza maneno yake, na nimekuwa naye karibu katika kila mikakati yangu ndani ya Simba. Hata muda mchache uliopita nimeongea nao kuwatakia kila la heri katika mashindano ya Shirikisho.”

 

Kuhusu kujiunga na Yanga. “Kwa Ufaransa, Kocha wa PSG hawezi kuwa kocha wa Marseille, hata Hispania Kocha wa Barcelona hawezi kuwa kocha wa Madrid. Nimepokea ofa miezi mitatu iliyopita, nitaangalia na wakala wangu, siwezi kuongea sana kuhusu hayo leo.” Kocha Didier Gomes Da Rosa.

Previous articleBREAKING OLE KUBAKI MAN UTD
Next articleHAJI MANARA:TUMEJIPANGA KUSHINDA MBELE YA AZAM