FEISAL:SUTI YANGU MBONA IPO FRESH,MWAKALEBELA ATAJWA

KIUNGO wa Yanga, fundi wa mipira migumu inayowashinda makipa Bongo akiwa nje ya 18, mzawa Feisal Salum amesema kuwa suti yake aliyotupia ni kali huku watu wakizusha kwamba ameazima kwa Mwakalebela, (Fredrick).

Heshima kubwa ilikuwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni mwanafamilia, mzalendo anayependa michezo alikuwepo kwenye usiku wa tuzo hizo na alipata muda wa kuzungumza na wachezaji pamoja na mashabiki kupitia vyombo vya habari kwa kuwa tukio lilikuwa mubashara Azam TV.

Oktoba 21 kwenye usiku wa Tuzo za  Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) 2021, Feisal alitupia suti moja matata ambayo ilizua gumzo kwa mashabiki pamoja na kwenye mitandao mbalimbali jambo ambalo lilimfanya kiungo huyo kuweka wazi kuwa hajaazima.

“Watu wanasema kuwa nimechukua sijui koti la Mwakalebela, (Makamu Mwenyekiti wa Yanga), hapana huo ni uzushi sijaazima nimechukua dukani na nilipoitupia nikaona ipo fresh.

“Kwangu mimi naona ipo fresh na haina tatizo lolote lile hivyo wale ambao wanasema kuhusu hilo hakuna ukweli kwani kwangu naona ipo fresh kabisa,” amesema kiungo huyo mwenye mabao mawili ndani ya Ligi Kuu Bara,

Kwenye usiku wa tuzo, kiungo huyo alisepa na tuzo mbili moja ikiwa ni ile ya Mchezaji Bora wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) pamoja na ile tuzo ya kuwa ndani ya kikosi bora cha Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.