
TWIGA STARS YAKIRI KUFANYA MAKOSA,KESHO KUFANYA KWELI
KOCHA wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime, amesema walifanya makosa kwenye mchezo uliopita wakiwa nyumbani na sasa wanakwenda kuwafunga Namibia wakiwa kwao, kesho Jumamosi. Twiga Stars walichapwa 2-1 na Namibia kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kwenda Afcon mwakani, kwenye mtanange uliochezwa Jumatano Uwanja wa Mkapa, Dar. Akizungumza na Championi Ijumaa,…