
NABI AMPA KAZI HII MAYELE YANGA
KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ametoa majukumu mazito kwa wachezaji wa timu hiyo, akiwemo kinara wa mabao, Fiston Mayele kwa kuhakikisha wanatupia mabao ya kutosha katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi. Nabi ametoa kauli hiyo baada ya kurejea kwa ligi kufuatia kumaliza mechi za Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) huku wakiwa na kumbukumbu za matokeo ya suluhu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mbeya City kabla ya ligi kusimama kupisha Shirikisho. Yanga inaongoza ligi ikiwa…