
CAF YAURUHUSU UWANJA WA BENJAMIN MKAPA KUTUMIKA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa kutumika kwa michezo inayosimamiwa na Shirikisho hilo baada ya Ukaguzi uliofanywa na Wakaguzi wa CAF mnamo Machi 20, 2025. Taarifa ya leo Machi 28, 2025 iliyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imeeleza kuwa CAF inaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea…