SIMBA YAPATA TUZO,YAWAPOTEZA YANGA

LEO Juni13,2022 Klabu ya Simba imeweza kupewa tuzo yake baada ya kuwapoteza wapinzani wao wa jadi Yanga kwenye mchakato wa kura. Ni Tuzo ya Klabu Bora kwenye Mitandao ya Kijamii Tanzania ambayo imetolewa na kampuni ya Serengeti Bytes. Mbali na watani zao wa jadi Yanga pia Simba imeweza kuwashinda kwa kura Azam FC, Mbeya City, Ruvu…

Read More

RATIBA YA LIGI KUU BARA BONGO LEO

 LEO Juni 13 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea baada ya mapumziko kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2023 zinazotarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast. Ni mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa leo ikiwa ni mzunguko wa pili na wa kufungia hesabu kwa msimu wa 2021/22. Mtibwa Sugar itawakaribisha Ruvu Shooting itakuwa ni Uwanja wa Manungu. Mchezo…

Read More

GLOBAL FC YATOSHANA NGUVU NA BONGO MOVIES

TIMU ghali Bongo ya Global FC inayomilikiwa na Kampuni ya Global Group iliweza kuonyesha ubabe wake mbele ya timu ya Bongo Movie kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Shule ya Msingi Muhimbili jana. Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ulichezwa mchezo mkubwa ambapo Global FC walianza kupata bao la…

Read More

MCHONGO MZIMA WA AZIZ KI UMECHORWA NAMNA HII

SAKATA la usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Stephen Aziz Ki, limezidi kuteka hisia za wapenda soka wengi hapa nchini, baada ya vigogo Simba SC na Yanga SC kuhusishwa naye. Kiungo huyo anayetumia zaidi mguu wa kushoto awapo uwanjani, inaelezwa kwamba tayari amemalizana na Yanga ambayo imetumia kiasi cha shilingi milioni 650 kumpa…

Read More

TEN HAG NA MTEGO WA USAJILI MAN U

DIRISHA la usajili limefunguliwa rasmi tangu, Juni 10, mwaka huu na litafungwa Septemba Mosi mwaka huu ikiwa ni wakati muhimu hasa kwetu kama Manchester United kwa kuhakikisha tunafanya maboresho. Jana Manchester United ilithibitisha rasmi kuachana na nyota wake 11 huku nje ya hao kuna wengine pia wanaweza kuondoka kikosini hapo.  Katika nyota ambao imethibitisha kuachana…

Read More

KOCHA KAIZER CHIEFS AMALIZANA NA SIMBA

BAADA ya kufanya mazungumzo mazito na mabosi wa Simba SC, inaelezwa kwamba kocha wa zamani wa Kaizer Chiefs, Stuart Baxter, wamefikia makubaliano mazuri, lakini ameomba kwanza kurejea kwao Uingereza. Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na England U19, juzi alifanya mazungumzo na mabosi wa Simba kwa ajili ya kukamilisha dili…

Read More

HUYU HAPA ANATAJWA KUWA KOCHA MPYA SIMBA

INAELEZWA kuwa mabosi wa Simba wapo kwenye mazungumzo na Stuart Baxter aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs  Kabla ya kufungashiwa virago vyake huko ili aweze kubeba mikoba ya Pablo Franco. Kwa sasa Simba ipo kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya ambapo CV zinatajwa kuwa zaidi ya 100 mezani kwa mabosi hao ambao wapo kwenye hatua za mwisho…

Read More

AZAM FC WAJA NA HESABU MPYA KABISA

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa sasa hesabu zao ni kwa msimu ujao kurejea kwa kasi na nguvu zaidi. Hizi zinakuwa ni hesabu mpya za Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zao za nyumbani. Tayari matumaini ya kutwaa mataji ndani ya Azam FC yameyeyuka kwa kuwa wamefungashiwa virago kwenye Kombe…

Read More

CHAMA KARUDI ILA BADO HAJAWA FITI

LICHA ya kuanza mazoezi ndani ya kikosi cha Simba kiungo Clatous Chama bado hajawa fiti kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu akitibu majeraha ya enka. Nyota huyo wa Simba kwa sasa yupo Bongo baada ya kurejea kutoka Zambia Julai 10 ambapo alikuwa huko akipewa matibabu ya enka ambayo aliiumia kwenye mchezo wa dabi dhidi…

Read More