BEKI JOASH ONYANGO APEWE ULINZI

MZUNGUKO wa dunia unavyozidi kwenda na matukio yanaongezeka na kwenye ulimwengu wa mpira kila wakati kumekuwa kuna mabadiliko ambayo yanatokea. Ndani ya kikosi cha Simba kuna beki wa kazi Joash Onyango ambaye amekuwa akionekana kwenye uvurugaji mara nyingi jambo linalowavuruga mashabiki pamoja na viongozi kwamba asepe ama abaki. Licha ya yote hayo beki huyo anahitaji…

Read More

UTAWALA WA WAGENI UTAZAMWE KWA UMAKINI

MUDA mchache wanasema mambo ni mengi ila ili yote yaende kwa umakini jambo la muhimu kuzingatia ni mpangilio kwenye kila hatua. Ni kuanzia Singida Big Stars ambao wamekuwa na msimu mzuri ndani ya Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza wanapaswa kuwa na mwendelezo. Kwa sasa Singida Big Stars inaitwa Singida Fountain Gate FC hivyo…

Read More

MUDA WA KAZI KWA AJILI YA MSIMU UJAO NI SASA

NYAKATI zinakuja na kupita na sasa ni wakati wa maandalizi ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote baada ya mabingwa wa ligi ambao ni Yanga kutangazwa. Ipo wazi kuwa kesi ya ubingwa kwenye kila eneo kuanzia Ligi Kuu Bara, Azam sports Fedaration mpaka suala la tuzo zote zimefungwa. Tumeona namna…

Read More

MAANDALIZI YA MSIMU MPYA YAANZE MAPEMA

BAADA ya kusimama kwa muda kupisha ratiba ya mashindano ya kimataifa, Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2022/23 ilirejea rasmi Juni 6 Jumanne kwa michezo nane kupigwa kwenye viwanja mbalimbali nchini. Kufuatia matokeo ya Juni 6 kila mmoja alianza kuona picha kamili baada ya kesi ya ubingwa kufungwa mapema na Yanga kufanikisha malengo yao. Yanga…

Read More

MAAJABU YA SOKA, MZUNGUKO WA 29 UMEACHA MENGI

HUWEZI kuzuia mvua kunyesha kwa namna yoyote ile wakasema acha inyeshe tuone panapovuja. Soka lina maajabu yake na mzunguko wa 29 ulikuwa noma kinomanoma. Kwenye Ligi Kuu Bara wakati wa lala salama rekodi mpya zimeandikwa kwa timu kupata matokeo ambayo yameacha mshtuko huku wachezaji wakiweka rekodi zao. Hapa tunakuletea namna kazi ilivyokuwa mzunguko wa pili…

Read More

ZIMETUPIA MABAO MENGI BONGO

MTIFUANO mkubwa kwa wachezaji kusaka pointi tatu ndani ya uwanja unabebwa na kasi ya kuzitungua nyavu za walinda mlango ndani ya uwanja. Suala la kufunga ni muhimu ambapo kwa msimu wa 2022/23 mabingwa wa ligi ni Yanga. Kila timu ina mbinu zake kwenye kusaka ushindi na kuamua matokeo jambo linalofanya kila kitu kuwa kama ambavyo…

Read More

HAKUNA KAZI NYEPESI MUHIMU KUJITOA

TAYARI kete ya kwanza imeshachezwa na kila mmoja ameona namna hali ilivyokuwa kwenye mchezo wa fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika. Leo msafara wa Yanga umeanza safari kueleka Algeria iwe ni safari njema na yenye mafanikio kwenu wawakilishi wa Tanzania kimataifa. Hakuna ambaye alikuwa amebeba matokeo uwanjani kwenye mchezo wa fainali ile ya…

Read More

YANGA WAPENI FURAHA WANANCHI INAWEZEKANA

WAKATI mwingine wa kuendeleza furaha kwa familia ya michezo inakuja siku ambayo Afrika itakuwa ikifuatilia habari za dakika 90. Ni dakika 90 zenye maamuzi ya dakika 90 za mwisho kwa Yanga kwenye mchezo wa fainali ya kwanza hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika. Kila mmoja anatambua kazi iliyopo mbele sio ndogo kutokana na ukubwa wa…

Read More

NGOMA ILIKUWA NZITO KWA WAKULIMA, JANGWANI WAKAPETA

KILA mmoja anafuata njia zake ambazo zitampa mafanikio akikwama kidogo kupotea ni hatua inayofuata asipojipanga itakuwa kazi nyingine. Ilikuwa hivyo Uwanja wa Liti, njia za Singida Big Stars wakulima wa alizeti njia ziliwagomea na zile za Yanga zikawapa ushindi baada ya dakika 90. Ngoma fainali ya Azam Sports Federation itakuwa ni Azam FC v Yanga,…

Read More

DARASA LA YANGA KIMATAIFA NI KWA WOTE

KASI ya Yanga kwenye mashindano ya kimataifa ni darasa huru kwa kila mmoja apate kujifunza namna ya kutumia bahati na nafasi inayotokea. Hakuna timu ambayo haipendi kupiga hatua kila siku na kuandika rekodi mpya na nzuri hilo lipo wazi hivyo kwa sasa mfano bora wa kuzungumzia kwenye kizazi cha sasa ni Yanga. Mfumo ambao wameutumia…

Read More

RUVU SHOOTING TUTAONANA BAADAYE, KUNA KUSHUKA DARAJA

NI rasmi timu ya Ruvu Shooting imeshuka daraja na haitakuwa sehemu ya timu za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24 huku timu za Polisi Tanzania, Mtibwa Sugar na KMC zikipambania hatma yao kwenye michezo miwili waliyobakisha kumaliza ligi. Kwa misimu ya hivi karibuni Ligi Kuu Bara imekua na ushindani mkubwa ambapo uwekezaji mkubwa uliofanywa…

Read More

KAPOMBE BADO HAJAPATA MBADALA WAKE SIMBA

SHOMARI Kapombe beki wa kazi ndani ya kikosi cha Simba ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Roberto Oliveira. Pasi yake ya sita kwenye ligi ilikuwa dhidi ya watani wa jadi, Yanga Uwanja wa Mkapa. Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-0 Yanga. Ikiwa hatakuwa fiti hapo ni pasua kichwa kwa…

Read More

WAKALI WA PASI ZA MWISHO BONGO HAWA HAPA

KWENYE mitupio ya mabao ambao hutazamwa kwa ukaribu yule mtu wa mwisho kutokana na kazi anayofanya ndani ya uwanja katika kutupia. Ipo wazi kwamba mabingwa wa ligi msimu wa 2022/23 ni Yanga ambao wametwaa ubingwa huo wakiwa na pointi 74. Yanga ina mechi mbili mkononi za kukamilisha mzunguko wa pili. Haitokei bahati mbaya ngoma ikazama…

Read More

YANGA KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO

USIOGOPE  kukabiliana na magumu kwa kuwa yanakukomaza uwe imara zaidi hivyo itakuwa hivyo kwa wawakilishi wa Tanzania Yanga kwenye anga la kimataifa. Ushindi wa mchezo wa kwanza haina maana kwamba kazi imegota mwisho bado kuna safari nyingine kukamilisha mwendo wa kuifuata fainali. Nyumbani ilikuwa furaha kwa kuwa kila mmoja aliona namna wachezaji walivyocheza kwa kujituma…

Read More

BANDA KAJENGA KIBANDA NDANI YA MSIMBAZI

KIUNGO wa Simba Peter Banda ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 amejenga kibanda chake mwenyewe kwa kushindwa kuonyesha makeke yake ndani ya uwanja. Moja ya sababu kubwa iliyofanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu ni kupambania hali yake kutokana na kutokuwa fiti kwa muda mrefu. Banda hana uhakika wa kuanza kikosi cha…

Read More