MTIBWA SUGAR YAPANIA KUVUNJA REKODI YA VINARA WA LIGI
UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umebainisha kuwa, kikosi chao kipo tayari kuvunja rekodi ya Yanga ya kutopoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Februari 23, mwaka huu ambapo Mtibwa watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro. Ikumbukwe kuwa, Mtibwa Sugar wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo kwa mabao 3-1 pamoja na kutolewa hatua ya…