IHEFU KUIKABILI NAMUNGO LEO UWANJA WA UHURU

BAADA ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting msimu wa 2022/23 kwa kufungwa bao 1-0, Agosti 19,2022 Ihefu ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Namungo FC, Uwanja wa Uhuru. saa 10:00 jioni.

Ihefu inanolewa na Kocha Mkuu Zuber Katwila ambaye aliibuka hapo baada ya kubwaga manyanga ndani ya Mtibwa Sugar leo ana kibarua cha kusaka ushindi kama ambavyo Namungo FC nao wanahitaji.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Namungo walianza kwa kuambulia sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ofisa Habari wa Ihefu FC, Peter Andrew ameweka wazi kuwa wamefanyia kazi makosa yao na leo wanahitaji ushindi.

“Makosa ya mchezo uliopita tumefanyia kazi na tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji furaha hivyo wasikate tamaa bado kazi inaendelea, ” amesema