Home Sports KOCHA NABI AKUBALI UWEZO WA NYOTA WAKE

KOCHA NABI AKUBALI UWEZO WA NYOTA WAKE

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameweka wazi kuwa viwango vya wachezaji wake ambavyo wameonyesha kwenye mechi mbili amevutiwa navyo na anahitaji waweze kuongeza zaidi.

Katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Yanga iliweza kushinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na iliweza kushinda pia mabao 2-1 mbele ya Polisi Tanzania ilikuwa kwenye mchezo wa ligi.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Fiston Mayele huku lile la Simba likifungwa na kiungo Pape Sakho.

Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya Coastal Union unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Agosti 20.

Kocha huyo amesema:”Tumekuwa na muunganiko mzuri kwenye kikosi hususani wachezaji wapya wameweza kuingia kwenye mfumo mapema na wanafanya kazi nzuri.

 “Nimevutiwa sana namna ambavyo kikosi changu kimeweza kuonyesha uwezo mkuwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania,” amesema Nabi.

Coastal Union watawakaribisha Yanga wakiwa wametoka kushinda kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya KMC baada ya ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kusoma Coastal Union 1-0 KMC.

Previous articleIHEFU KUIKABILI NAMUNGO LEO UWANJA WA UHURU
Next articleMBINU YA SIMBA KUTWAA UBINGWA IPO HIVI