ARSENAL YATEMBEZA KICHAPO CHA 4G

UWANJA wa Emirates, Arsenal imeshinda jumla ya mabao 4-2 dhidi ya Leicester City ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu England.

Ushindi huo unawafanya washika bunduki hao kusepa na pointi tatu mazima kwa mabao ya Gabriel Jessus dk ya 23 na 35,Granit Xhaka dk 55 na Gabriel Martinell dk ya 75.

Kwa upande wa Leicester City ni bao la kujifunga la William Saliba na dk 53 na James Maddson dk 74.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha pointi 6 ikiwa nafasi ya pili huku Leicester City ikiwa nafasi ya 14 na pointi moja.