PARIS Saint Germain,(PSG) wamefanikiwa kufungua msimu wa 2022/23 kwa kutwaa taji la Trophee des Champions ambapo Lionel Mess,Neymar Jr na Sergio Ramos waliweza kufanya kweli.
PSG waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nantes kwenye mchezo uliokuwa ni wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2022/23.
Kwenye mchezo huo mabao ya PSG yalifungwa na Messi ambaye alitupia bao moja dk ya 22,Neymar alitupia mabao mawili ilikuwa dk ya 45 na 82 kwa mkwaju wa penalti na Ramos yeye alitupia bao dk ya 57 ilikuwa ni Julai 31.
Staa mwingine ambaye ni Kylian Mbappe yeye alikosekana kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa na adhabu ya kadi.
Na mchezaji mmoja wa Nates alionyeshwa kadi nyekundu dk ya 81 anaitwa Jean-Charles .
Huu ni mchezo wa kwanza wa ushindani kwa msimu wa 2022/23 na mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu Christopher Galtier na linakuwa ni taji la tisa kwa PSG ndani ya miaka 10.