BAYERN Munich inatajwa kuwania saini ya Harry Kane ambaye anacheza ndani ya Spurs inayoshiriki Ligi Kuu England.
Kane mkataba wake ndani ya Spurs umebakiza miaka miwili hivyo ikiwa watakuwa wanahtaji saini yake wanapaswa kuvunja mkataba wake mazima.
Nyota huyo ana umri wa miaka 28 aliletwa duniani mwaka 1994 hivyo bado ana umri wa kuendelea kupambana na kuonyesha kipaji chake.
Alitua ndani ya Spurs mwaka 2004 akiwa na timu ya vijana hivyo ametumia jumla ya miaka 18 akiwa ndani ya Spurs mshambuliaji huyo raia wa England.