Home Sports BEKI MPYA ATAMBULISHWA SIMBA LEO

BEKI MPYA ATAMBULISHWA SIMBA LEO

RASMI leo Julai 22 Simba imemtambulisha beki mpya ambaye atakuwa kwenye kikosi chao kwa msimu wa 2022/23 katika mashidano ya kitaifa na kimataifa akichukua mikoba ya Pascal Wawa ambaye aliachwa rasmi na Simba.

Simba wenyewe wamemuita beki kisiki wa kuzuia mipira ya juu na chini, beki bora na mwenye uwezo wa kucheza kwenye kikosi chao anaitwa Mohamed Ouattara raia wa IvoryCoast.

Beki huyo aliwahi kufanya kazi na Kocha Mkuu wa Simba Zoran Maki kwenye Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco na Al Hilal ya Sudan.

Jumatatu aliwasili kambini Misri na leo Julai 22 ametambulishwa rasmi akiwa amesaini dili la miaka miwili.

Previous articleKANE AINGIA ANGA ZA BAYERN MUNICH
Next articleISHU YA UWANJA YAMSHANGAZA KOCHA,KESHO STARS KAZINI