RAIS wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amewakabidhi kadi za uanachama kwa Wasanii Faustina Mfinanga wanamjua kwa jina la Nandy na William Lyimo wengi wanauita Nenga.
Wawili hao kwa sasa ni mwili mmoja baada ya kukamilisha kufunga pingu za maisha wikiendi hii.
Mbali na kadi hizo pia Injinia Hersi aliwakabidhi fedha Tsh Mil 5,ikiwa ni pongezi kwa mashabiki hao wa Yanga.
Rais huyo ambaye amechaguliwa hivi karibuni alikuwa mmoja ya watu maarufu waliohudhuria sherehe ya mastaa hao wa Bongo Fleva iliyofanyika Mlimami City, Dar es salaam.
Nandy na Billnass wamefunga pingu ya maisha katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach Dar na kuhudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki.
Ikawe kheri na baraka kwenu katika hatua nyingine.