MTANZANIA Abdi Banda amepata changamoto mpya kwa ajili ya kuonyesha uwezo wake kwa msimu mpya wa 2022/23.
Banda ambaye ni nyota wa zamani wa Baroka FC ya Afrika Kusini amesaini mkataba wa miaka 2 kuichezea timu ya Chippas United inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Kabla ya kujiunga na Chippas Banda aliwahi kukipiga pia Highland Park na msimu wa 2021/22 alikuwa ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar ya Tanzania.
Banda amesema:-“Nimesaini miaka miwili. Nafurahi nimerudi, naomba Watanzania wote waniunge mkono na kunipa sapoti sababu sio kazi nyepesi.
“Kikubwa watusapoti na sisi wazawa. Wategemee ujio mwingine na kuona tofauti kubwa,” amesema