MERIDIANBET WAAHIDI KUENDELEA KUSAPOTI SOKA LA WANAWAKE!

KAMPUNI ya Meridianbet imeendelea na utamaduni wake wa kushirikiana na jamii, na kuwatengenezea vijana hamasa ya kuendeleza vipaji vyao. Kama sehemu ya utaratibu wake wa kila Mwezi kampuni hii imeandaa bonanza la soka la wanawake lililofanyika Jijini Dar es Salaam, wikendi iliyopita.

Meridianbet iliamua kuzishika mkono klabu nne za madaraja ya chini za Mkoa wa Dar kwa kuzipatia vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mipira katika bonanza wikiendi iliyopita kwenye uwanja wa Chuo cha Ardhi.

Timu nne zilizoalikwa kushiriki, Temeke Sisters, Masala Princess, Aman Queens na Sayari Queens, na Aman Queens aliibuka bingwa wa bonanza hilo, mshindi wa pili alikuwa Temekea Sisters na Masala Princess walishika nafasi ya tatu na Sayari Queens wakishika nafasi ya nne.

Mshindi wa kwanza alipata jezi seti moja na mipira miwili na kombe, huku mshindi wa pili akiondoka na jezi seti moja na mipira miwili, mshindi wa tatu alizawadiwa jezi seti moja na mpira mmoja na mshindi wa nne alichukua mipira miwili na gloves za golikipa.

Diwani wa Viti Maalumu Wilaya ya Kinondoni Grace, Mkumbwa, ambaye alialikwa kama mgeni rasmi kwenye bonanza hilo moja ya kitu alichozungumza kabla ya kutoa zawadi hizo aliwatia moyo wachezaji na kuwataka kutokata tamaa na akitoa ahadi ya kupigania wanachokifanya.

Kauli ambayo ilifanana na aliyoitoa balozi wa Meridian muimbaji wa Bongo Fleva, Fobby. Kocha wa Masala Princess Mbwana Mbaraka alishukuru kwa niaba ya makocha wenzake na kusema kilichofanywa na Meridian kitabaki mioyoni mwao.

Mwakilishi wa Idara ya Masoko ya Meridianbet, Twaha Ibrahimu alisema wamewashika mkono wachezaji hao kwa kutambua vipaji na nguvu yao kubwa wanayoitumia kwenye soka na kuahidi kuandaa bonanza lingine litakalofana zaidi.