SIMBA KAMILI KUIVAA KMC

SELAMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Simba imetoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Matola amesema:”Mchezo wetu tunajua kwamba utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kuweza kuona tunapata pointi tatu muhimu.

“Kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kupata ushindi na wachezaji wapo tayari hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kuona burudani,”.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ina pointi 54 baada ya kucheza mechi 26.

Mabingwa wa ligi ni Yanga ambao wamecheza mechi 27 na wana pointi 67 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine.

Imeandikwa na Dizo Click.