BEKI SIMBA YAMKUTA HUKO

BEKI wa Simba, Henoc Baka amefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga kichwa mchezaji wa Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kutokana na kitendo hicho beki huyo alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na kumfanya akose mchezo wa Simba uliofuata dhidi ya Namungo FC.

Mbali na adhabu ya mechi tatu pia beki huyo amepigwa faini ya shilingi milioni moja kutokana na kitendo cha kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Oktoba 31, Uwanja wa Mkapa na dakika 90 zilikamilika kwa ubao wa kusoma Simba 0-0 Coastal Union.

Hii ni kwa mujibu wa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania,(TPLB) katika kikao chake cha Novemba 5,2021.