LEO Juni 5,2022 timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17 inacheza mchezo wa marudio kuweza kuwania kufuzu Kombe la Sunia.
Mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini, U 17 ya Tanzania ilishinda kwa mabao 4-1 hivyo leo wanakamilisha dk 90 za mchezo wa pili.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika na imekuwa Tanzania U 17 0-0 Cameroon, U 17,((Agg 4-1)) Uwanja wa Amaan.
Mchezo ulichelewa kuanza kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda sawa.