POULSEN AKUBALI UWEZO WA WACHEZAJI WAKE

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa uwezo wa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi hicho ni mkubwa na anaamini kwamba watampa matokeo chanya kwenye mechi za kimataifa.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Poulsen alisema kuwa kila mchezaji ambaye ameuita kikosini alipata muda wa kumfuatilia na kuona uwezo wake na wapo wengine ambao walikuwa pamoja kwenye kikosi hicho waliposhinda dhidi ya Benin.

“Wachezaji wengi ni wazuri na uwezo wao unanifurahishwa kwa kuwa kila siku wanazidi kuimarika hivyo sina mashaka nao kwa mechi zetu ambazo tutacheza.

“Tuna mechi ngumu mbele yetu na tunajua kwamba tutaanza nyumbani ambapo rekodi zinaonyesha kuwa ukiweka kando ule mchezo dhidi ya Benin kuna mechi ambazo tulifanya vizuri hivyo ni muda wa mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega na timu yao,” alisema Poulsen.

Kwa sasa timu ya taifa ya Tanzania, imeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia ambapo watakuwa na mchezo Novemba 11, dhidi ya DR Congo, Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye mazoezi ni pamoja na Edward Manyama,Mzamiru Yassin, Kibwana Shomari na Dickson Job.

 

ReplyForward