ISHU YA CHAMA KURUDI BONGO,YANGA,SIMBA ZATAJWA

KIUNGO bora wa zamani wa Simba, Clatous Chama anatajwa kurudi tena Bongo huku timu mbili za Kariakoo, Simba na Yanga zikitajwa kuwania saini yake.

Chama msimu wa 2020/21 alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu na pia alitwaa tuzo ya kiungo bora ikumbukwe pia kwa msimu wa 2019/20 alitwaa tuzo ya kiungo bora pamoja na mchezaji bora wa msimu ambapo kwa msimu uliopita ipo mikononi mwa nahodha wa Simba John Bocco.

Alisepa Bongo na kuibukia Morocco ambapo kwa sasa anakipiga ndani ya RS Berkane na amekuwa akitajwa kurudi tena kwa mara nyingine kwa ajili ya kuitumikia Simba huku tetesi zikitaja kuwa anaweza kurudi na kucheza Yanga.

Hivi karibni Chama alipoulizwa kuhusu kurudi Tanzania na kucheza Simba alisema kuwa inawezekana kuwa hivyo ikiwa Simba watamfuata na kumpa ofa kwa kuwa anaiheshimu timu hiyo na ni kubwa.

“Inawezekana kurudi ikiwa Simba watanifuata kwa kuwa ni timu kubwa hivyo lolote linaweza kutokea kwa kuwa kazi yangu mimi ni mchezaji.

Kuhusu kucheza Yanga pia aliwahi kusema kwamba anaweza kucheza lakini mpaka ofa itakapomfikia.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa moja ya wachezaji ambao anawakubali na wana uwezo ni pamoja na Chama na anaota kwamba siku moja watafanya naye kazi pamoja.

“Nimemmiss sana huyu mwamba na naota siku moja Insha’Allah tutakuja kufanya kazi pamoja tena,”