ISHU YA TAMMY KURUDI ENGLAND NGOMA NZITO

IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa kikosi cha AS Roma, Tammy Abraham yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya kikosi cha Arsenal kinachoshiriki Ligi Kuu England huku bosi wake akiweka wazi kwamba hadhani kama anaweza kurudi huko.

Roma ilimsajili Tammy msimu uliopita akitokea Chelsea na ilikuwa ni baada ya Kocha Mkuu Jose Mourinho kujiunga na timu hiyo.

Ni kwa mara ya kwanza Tammy amecheza ndani ya Serie A na amekuwa kwenye mwendo mzuri na kufanya kazi yake ya kucheka na nyavu akiwa ametupia mabao 25 katika michuano yote huku kwenye ligi akiwa amefunga mabao 15.

Mourinho amesema:”Alichagua na hii ni baada ya kuniamini mimi lakini sasa kama anataka kurudi England sidhani kama atafanya hivyo na kama anataka kurudi basi tutajua baadaye,”