SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa magumu ambayo wanayapitia kwa sasa yana muda kwa kuwa wanapambana kurudi kwenye ubora uliozoeleka.
Ikiwa imecheza mechi tano imeshinda mechi tatu na kukusanya sare mbili ndani ya msimu wa 2021/22 na kinara wa utupiaji ni Meddie Kagere mwenye mabao mawili.
Akizungumza na Spoti Xtra, Matola alisema kuwa wanatambua kwamba wanapitia kipindi kigumu ila kuna mwisho kwa kuwa kinachowasumbua kipo wazi.
“Ipo wazi kwamba kwa sasa tunapitia kwenye wakati mgumu lakini haya mapito yana mwisho hayatadumu siku zote. Nilikuwa mchezaji wa Simba na niliwahi kukutana na mambo kama haya.
“Licha ya hivyo hata msimu uliopita pia tulipitia kwenye kipindi kama hichi lakini mwisho wa siku tukarejea kwenye ubora na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, mashabiki wasikate tamaa waendelee kuwa nasi kama ambavyo kwa sasa wanafanya,”alisema Matola.