REKODI ZA MASTAA WA YANGA V SIMBA,KIKOSI KAMILI

ULE utundu wa kutamba sasa unakaribia lakini kwa jeshi hili la Yanga na Simba, Aprili 30 unadhani nini kitatokea?

Ngoma inatarajiwa kupigwa kwa watani hawa wa jadi ambapo vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 54 na mabao 35 na Simba wao wana pointi 41 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 23.

Hapa tunakuletea jeshi la Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na Pablo Franco ambaye ni kocha wa Simba:-

Yanga

Diarra

Alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wake uliopita mele ya Namungo na alitunguliwa bao na mchezaji wa zamani wa Simba Shiza Kichuya.

Kwenye dabi ya mzunguko wa kwanza ya sare ya bila kufungana alikuwa langoni pia huyu kipa wa Yanga.

Diarra Djigui kacheza mechi 16,dk 1,440 kafungwa mabao 6 na ana cleen sheet 10.

Djuma

Hatma yake itaamuliwa leo kama anaweza kuanza ama la kwa kuwa aliumia kwenye mchezo dhidi ya Namungo ni beki wa kupanda na kushuka.

Djuma Shabani yeye katupia mabao 3 asisti 4 kwenye mechi 17 na kayeyusha  dk 1,515

Kibwana

Mechi 9 kacheza na kutumia dk 677 ana pasi moja ya bao, huyu stori zake zipo kwenye kichwa cha Bernard Morrison wa Simba namna alivyogandwa mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Bangala

Yannick Bangala jitu fulani hivi limekwenda hewani halafu miguu ya kazi akiwa ana asisti 1 kwenye mechi 16 dk 1,515 kasepa nazo.

Mwamnyeto

Mzawa ambaye ni Nahodha Bakari Mwamnyeto kayeyusha dk 1,533 kwenye mechi 17 za ligi.

Aucho

Khalid Aucho mwili wake umejengekeka kimazoezi na amecheza  mechi 13 asisti 3 dk 1,239 yeye ni kiungo wa kutibua na kutengeneza.

Sure Boy

Ngumu kuamini kwmba atapenya kikosi cha kwanza lakini Salum Abouakhari ni miongoni mwa viungo ambao wameanza kuwa kwenye ubora.

Mechi aliyowaka zaidi ilikuwa mbele ya Azam FC alipopiga jumla ya pasi 41 na amecheza mechi 6 akitumia dk 454.

Moloko

Jesus Moloko ni mechi 14 kacheza kayeyusha dk 921 katupia mabao 4 na ana pasi 1 ya bao.

Farid

Farid Mussa ni mechi 15 kacheza akisepa na dk 721 kibindoni ana pasi moja.

Feisal

Kutoka kutokuwa fiti sasa karundi ni Feisal Salum amecheza mechi 17 katumia dk 1,415 katupia mabao 5 na pasi 3 za mabao.

Mayele

Fiston Mayele mzee wa kutetema akiwa ametupia mabao 12 kwenye mechi 20 na kayeyusha dk 1,565 ana asisti 3.

Simba

Mabingwa watetezi wa ligi Simba nao sio wanyonge wana watu wa kazi chini ya Pablo Franco ambaye ni kocha mkuu na kete yake huenda itakuwa namna hii:-

Manula

Air Manula anapenda kuitwa hivyo yeye ni Aishi Manula katumia dk 1,440 kwenye mechi 16 alikaa langoni kafungwa mabao 7 kwenye mechi 7 na amekuanya clean sheet 9.

Kapombe

Mwenye jukumu la kupiga mapigo huru na kumwaga maji ni Shomari Kapombe akiwa alionekana kwenye jumla ya mechi 14 akatoa pasi mbili za mabao na ni dk 1,242 kayeyusha.

Mohamed Hussein

Nahodha msaidizi wa Simba katumia dk 1,366 kwenye mechi 17 katupia bao moja na katoa pasi mbili za mabao yeye ni beki wa kupanda na kushuka.

Inonga

Henock Inonga beki wa kazi ngumu ndani ya Simba amecheza mechi 13 na kasepa na dk 1,055.

Wawa

Pascal Wawa beki mwili jumba mwenye uzoefu wa kutosha huku mwili wake ukiwa na michoro kibao amecheza mechi 8 kasepa na dk 632.

Mkude

Huyu ni kiungo mkongwe akiwa na uzoefu wa kutosha anaitwa Jonas Mkude kacheza mechi 12 dk 767 asisti 2 msimu huu.

Sakho

 Pape Sakho mzee wa kunyunyiza yeye katumia dk 669 kwenye mechi 13 katupia mabao 2 ana pasi  1.

Kanoute

Jasiri mwenye ukatili kwenye miguu yake ila sura ya upole kaenda hewani kimtindo wanamuita Sadio Kanoute dk 668 mechi 8 bao 1.

Kagere

 Meddie Kagere amecheza mechi 19 katumia dk 983 katupia mabao 7 na pasi moja ya bao.

Chama

Hana zali la kuwa mkali mbele ya Yanga lakini ni kiungo bora wa muda wote ndani ya ligi anaitwa Clatous Chama kacheza mechi 8 katupia mabao 3 kasepa na dk 510.

Morrison

Mzee wa kuchetua kacheza mechi 11 katupia bao 1 na ametoa pasi 2 za mabao.

@Dizo_Click.