WAKALA mkubwa duniani Mino Raiola amelazimika kujibu mitandaoni akiwa kwenye kitanda kukanusha taarifa ambazo zimesambaa zikidai kwamba amefariki.
Taarifa ziliibuka nyumbani kwao Italia ambapo zilieleza kuwa wakala huyo mkubwa amefariki baada ya kuugua.
Ikumbukwe kwamba miongoni mwa wachezaji ambao anawasimamia ni pamoja na Paul Pogba,Erling Haaland ambao ni wachezaji wakubwa.
Kumekuwa na meseji nyingi za faraja ambazo zilikuwa zinatumwa kuhusu wakala huyo ikiwa ni pamoja na meseji moja kutoka miamba wa La Liga, Real Madrid.
Kutoka kitandani wakala huyo aliandika:”Nikiwa katika hali mbaya ya kiafya,hii ni mara ya pili sasa ndani ya miezi minne wameniua,wanaonekana pia wanaweza kufufua,”.