LIGI KUU ENGLAND, C.PALACE 0-0 LEEDS UNITED

UWANJA wa Selhurst mchezo umekamilika kwa Crystal Palace 0-0 Leeds na kuwafanya waweze kugawana pointi mojamoja kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Ulikuwa ni mchezo wa kujilnda kwa timu zote mbili na hawakuweza kutengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni mgumu kwa kila timu.

Leeds wamekosa pointi tatu ambazo zingewaongozea nguvu ya kujinasua kutoka kwenye hatari ya kuweza kushuka daraja.

Illan Meslier amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo ambapo aliweza kuokoa jumla ya hatari 7 ndani ya dakika 90 ambazo alicheza zilizopigwa na wapinzani wao C.Palace.

Kocha Mkuu wa Leeds,Jesse Marsch amesema kuwa alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda lakini amekwama kupata pointi tatu muhimu.

Patrick Vieira ,Kocha Mkuu wa C,Palace amesema kuwa matokeo ambayo amepata kwake ni furaha na anawapongeza wachezaji wake.

Leeds ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 34 huku Palace ikiwa nafasi ya 14 pointi 38 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.