CITY NI NAMBA MOJA KIMATAIFA, WANAKIMBIZA

NDANI ya Ligi Kuu England Manchester City ni baba lao kwa kukusanya pointi nyingi tangu msimu wa 2018/19 mpaka msimu huu wa 2021/22.

Ni pointi 338 wamekusanya huku wanaowafuata wakiwa ni Liverpool ambao wana jumla ya pointi 337 na Chelsea ni namba tatu wakiwa na pointi 264 Manchester United ni namba nne wana pointi 257.

Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa hawakuwa bora mwaka mmoja uliopita kutokana na matatizo ambayo walikuwa wakipitia ila awali walikuwa wanakwenda sawa.

Leo Jumapili,Aprili 10 Uwanja wa Etihad, unatarajiwa kuchezwa mchezo kati ya Manchester City v Liverpool na mchezo wao uliopita pale Anfield ubao ulisoma Liverpool 2-2 City.

Pia leo nikumbukizi ya kuletwa duniani winga kutoka Senegal, Sadio Mane.