MANCHESTER UNITED KAMA ULIVYOSIKIA WAMECHAPWA HUKO

KLABU ya Everton imefufua matumaini ya kuweza kuwa na nguvu ya kubaki ndani ya Ligi Kuu England baada ya ushindi mbele ya Manchester United.

Ushindi ambao wamepata wa bao 1-0 Manchester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jioni ya leo una maana kubwa kwao kwa kuwa hawakuwa wanachohitaji zaidi ya pointi tatu.

Bao la ushindi kwa Everton limepachikwa na Anthony Gordon  ilikuwa ni dk ya 27 na kuifanya timu hiyo kubakiza pointi tatu nyumbani katika Uwanja wa Goodison Park.

Sasa Everton inafikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo huku United ikibakiwa na pointi zake 51 ipo nafasi ya 7.

Matumaini ya kuweza kumaliza ndani ya Top 4 kwa United yanazidi kuwa magumu kutokana na mwendo wa matokeo kuwa toauti na vile ambavyo wengi wanafikiria.

Manchester United iliweza kupiga jumla ya mashuti 12 huku mashuti manne pekee yakilenga lango na ni mashuti 7 yalipigwa na Everton huku matatu pekee yakilenga lango kwenye mchezo wa leo ambao United waliongoza kwenye suala la umiliki.