AZAM FC YACHAPWA 2-1 YANGA

UWANJA wa Azam Complex, dakika 90 za zimekamilika na Yanga inasepa na pointi tatu muhimu ikiwa ugenini.

Vinara hao wa ligi wanafikisha pointi 51 wamepindua meza kibabe baada ya kuanza wakiwa wanadaiwa bao moja kisha wakalipa na kuogeza bao lingine la ushindi.

Azam FC wanapaswa wajiliamumu wenyewe kwa kuwa walikosa nafasi za wazi tatu za kuweza kufung mapema kipidi cha kwanza kabla mambo hayajawa magumu kipindi cha pili

Rodgers Kola alifunga bao moja kwa Azam FC huku Djuma Shaban na Fiston Mayele wakitupia kwa Yanga.

Azama FC inabaki na pointi zake 28 ikiwa nafasi ya tatu huku nafasi ya pili ni Simba wenye pointi 37..