MUGALU,BERNARD MORRISON KIMATAIFA NI HABARI NYINGINE

NYOTA wawili wa Simba, Bernard Morrison na Chris Mugalu kwenye mashindano ya kimataifa ni habari nyingine kwa kuwa wameweza kufanya maajabu kwenye mechi ngumu kwa kushirikiana na wachezaji wengine.

 Morrison kwenye mashindano ya kimataifa kuanzia hatua ya mtoano ametumia dk 290 katupia mabao matatu na pasi mbili za mabao.

Chris Mugalu yeye amecheza mechi tatu kwenye hatua ya makundi akiwa ameyeyusha dk 123 na ametupia mabao mawili yaliyoivusha Simba hatua ya robo fainali ikiwa na pointi 10 kibindoni.

Mzee wa kukera Morrison ilikuwa mbele ya Red Arrows alitumia dk 90 Uwanja wa Mkapa alifunga mabao mawili na alikuwa nyota wa mchezo, ugenini mbele ya Red Arrows alitumia dk 56.

USGN ugenini alifunga bao 1 akitokea benchi na alitumia dk 26 pia alikuwa ni nyota wa mchezo baada ya kufunga ao lililoipa pointi moja Simba ugenini na Uwanja wa Mkapa mbele ya USGN alitumia dk 79 alitoa pasi mbili za mabao.

Alipokutana na RS Berkane ugenini alitumia dk 45 na alionyeshwa kadi moja ya njano, Uwanja wa Mkapa alitumia dk 28 na mbele ya ASEC Mimosas alisepa na dk 45.

Mugalu ni mechi tatu amecheza ilikuwa mbele ya RS Berkane dk 4, dk 37 mbele ya ASEC Mimosas na dk 82 mbele ya USGN.

Kwenye upande wa milingoti ni Aishi Manula ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Pablo Franco yeye aliweza kutimiza majukumu yake mbele ya USGN juzi walikwama kumtungua.