RASHID Nortey raia wa Ghana anatajwa kuwa kwenye hesabu za kusajiliwa na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 48 aada ya kucheza mechi 18 msimu wa 2021/22.
Nyota huyo anacheza katika Klabu ya Medeama inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana.
Rekodi zinaonyesha kuwa ni moja ya kiungo ambaye anafanya kazi kubwa kutimiza majukumu yake akiwa na umri wa miaka 26.
Hivi karibuni kocha wa Yanga, Nabi alisema kuwa kwenye suala la usajili ambacho huwa anakitazama ni uwezo wa mchezaji pamoja na uhitaji.
“Ikiwa utazungumzia kuhusu usajili ambacho kinatazamwa ni uwezo wa mchezaji pamoja na uhitaji ndani ya kikosi kwa sasa nina wachezaji wazuri ambao wanatimiza majukumu yao,” .