JESUS MOLOKO ANAIPIGIA HESABU NAMBA YAKE

KIUNGO wa Yanga, Jesus Moloko ambaye alikuwa nje kwa muda kutokana na kuwa na majeraha amesema kuwa kwa sasa yupo fiti na anahitaji kuanza kikosi cha kwanza.

Wakati alipokuwa nje kwa muda kiungo huyo mikoba yake ilikuwa mikononi mwa Said Ntibanzokiza,Farid Mussa na Chico Ushindi ambao walikuwa wakipewa majukumu na Kocha Mkuuu wa Yanga, Nasreddine Nabi.

Kwa sasa tayari nyota huyo ameshareja kikosini na kuanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzanke ambao wanajiaanda na mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC.

Kiungo huyo amesema:”Ninafurahi kuweza kurejea na kuanza mazoezi nina amini kwamba kuwa fiti kutanifanya niweze kurejea kwenye kikosi na kuendelea kutimiza majukumu yangu ndani ya timu.

“Kikubwa ni kuona kila siku ninakuwa bora na nilipokuwa nje nilikuwa naona namna hali inavyokwenda na nilikuwa ninafanya mazoezi binafsi ili kuwa imara,”.