ILIKUWA ni bonge moja ya mechi na upinduaji meza wa kipekee baada ya Leeds United kuwa nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers.
Mabao ya Jonny Otto dk 26 na Francisco Machado Trincao dk 45+11 yaliwapa uongozi kwa muda Wolverhampton na baada ya Raul Jimenez kuonyeshwa kadi nyekundu dk 53 meza iliweza kuanza kupinduliwa.
Mabao ya Jack Harrison dk 63,Rodrigo dk 66 huku msumari uliowapa pointi tatu ulipachikwa na Luke Ayling dk 90+1 na kufanya ubao wa Uwanja wa Molineux kusoma Wolverhampton Wanderers 2-3 Leeds United.
Ayling aliweza kuwa mchezaji bora wa mchezo huo wa Ligi Kuu England.