SIMBA WAKWEA PIPA KUWAFUATA ASEC

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa Simba leo Machi 18 wamekwea pipa kuwafuata wapinzani wao RS Berkane kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho.

Ni leo alfajiri kimeanza safari kwa ajili ya kwenda Benin kuikabili ASEC Mimosas ikiwa ni mchezo wa marudiano ambao unatarajiwa kuchezwa Jumapili, Machi 20,2022.

Simba itafikia Hotel ya Azalia Hotel De La Plage Benin iliyopo jijini Cotonou ambapo mchezo huo wa kundi D mchezo huo unatarajiwa kuchezwa.

Kwenye kundi D Simba inaongoza ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza mechi 4 na miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Yusuph Mhilu, Sadio Kanoute.

Pablo Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kimataifa.