LAUTARO Martinez nyota wa kikosi cha Inter Milan alivunja rekodi ya Klabu ya Liverpool kutopoteza mchezo wa ushindani katika mechi zake za Uwanja wa Anfield baada ya kuwatungua bao dakika ya 61.
Ni katika mchezo wa UEFA Champions League uliochezwa Uwanja wa Anfield ambao ulikuwa ni wa raundi ya 16 ukiwa ni mchezo wa pili.
Licha ya Liverpool kupoteza wanafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa kuwa mchezo wa awali walishinda mabao 2-0 Uwanja wa San Siro.
Alexis Sanchez alifanya makosa ambayo yaliigharimu timu yake ya Inter Milan jambo lililofanya aweze kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 63.
Alitolewa kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano na kuifanya Inter Milan kucheza ikiwa pungufu.