TAARIFA kutoka Geita Gold kuhusu mchezaji wao Erick Yema ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga imeeleza namna hii:-
“Siku ya Jumapili (Juzi) kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga baada ya kugongwa na mguu na mchezaji wa Yanga (Zawadi Mauya) alishindwa kuendelea na mchezo hali iliyotulazimu kuchukua ‘ambulance’ na kumkimbiza hospitali kwa uchunguzi.
“Erick bado hali yake si nzuri, vipimo vya X-ray na Utra Sounds vilivyofanyika hospitali ya Bugando, Mwanza na Waja Hospital hapa mjini Geita vimefanana hakuwa na tatizo lakini tumbo linaonekana kujaa hali iliyotufanya leo Jumanne tumrejeshe tena hospitali ya Bugando, Mwanza kwaajili ya uchunguzi zaidi.
“Sisi kama Geira Gold tunaamini ajali hutokea mchezoni japo usalama wa mchezaji mwenzako ndio jambo muhimu na la kwanza kabisa katika mchezo huu pendwa.
“Tunamuombea mchezaji wetu apone haraka na arejee mapema katika majukumu yake ya kawaida,”.
Mpira ni mchezo wa kiungwa.
Kwenye mchezo huo wa ligi, Yanga ilishinda bao 1-0 lilofungwa na Fiston Mayele dakika ya kwanza.