EVERTON YAPIGWA 5-0,YATABIRIWA KUSHIRIKI CHAMPIONSHIP

JAMIE Carragher amesema kuwa Klabu ya Everton ipo kwenye hatari ya kuwa katika Championship baada ya kukubali kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Spurs.

Frank Lampard ambaye ni Kocha Mkuu wa Everton ameshuhudia timu hiyo ikipoteza katika mechi nne za Ligi Kuu England.

Carragher ambaye ni mchambuzi ndani ya skysports amesema:”Ikiwa unaona timu inakuwa na matokeo mabaya nyumbani na ugenini jambo la haraka linalokuja ni kwamba ni dhaifu halafu walaini.

“Ninasema kwamba inaweza kurudi Championship lakini kwa Everton bado hawajawa tayari katika kupambana,”.

Watupiaji walikuwa ni Michael Keane dk 14 alijifunga,Son Heung-min dk 17,Harry Kane dk 37 na 55 na Sergio Reguilon dk 46 ilikuwa Uwanja wa Tottenham Hotspur.

Kwenye msimamo Everton ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 25.