YANGA KUIFUATA GEITA GOLD FULL MUZIKI

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zijazo na kurejesha shukrani kwa mashabiki ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi uwanjani.

Manara amesema:”Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya matokeo ambayo tunayapata kwenye mechi zetu za Kombe la Shirikisho pamoja na mechi za ligi.

“Ushindi huu unahanikizwa na kila Mwanayanga na kila shabiki, tunawapongeza na tunawashukuru kwa hili.

“Tunawasisitiza kwamba popote pale Yanga inapocheza viwanja vipendeze, wakazi wa Dar mmeanza kufanya jambo hili kwa umakini inapendeza.

“Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar wachezaji wamepewa mapumziko hadi kesho saa 10 tutakapoanza mazoezi, Ijumaa asubuhi tutakwenda Mwanza kwa ajili ya kuikabili Geita Gold.

“Maandalizi yapo vizuri hatuna majeruhi mpya kwa maana ya Kibwana Shomari, Ninja na Ngushi hawa tayari wameanza program ya mazoezi.

“Dickson Job na Feisal Salum wanatarajiwa kurejea uwanjani kwa kuwa tayari wamemaliza adhabu zao, Job amemaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu na Fei adhabu ya kadi tatu za njano imeisha,” amesema Haji.

Mchezo ujao wa Yanga unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Machi 6,2022.