KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco leo Februari 26 kimewasili salama mji wa Berkane.
Safari ya kuibukia Berkane ilianza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mohammed V uliopo Casablanca.
Simba ina kibarua cha kumenyana na Klabu ya RS Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, kesho Februari 27.
Ni katika kundi D ambalo vinara ni Simba wakiwa na pointi 4 wanakutana na RS Berkane wenye pointi tatu mchezo wao uliopita walipoteza mbele ya ASEC Mimosas Februari 20 kwa kufungwa mabao 3-1.
Simba imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya USGN ya Niger.