UJANJA WA NONGA NI UWANJA WA SOKOINE

    MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Mbeya City, Paul Nonga, ujanja wake wa kucheka na nyavu ni kwenye Uwanja wa Sokoine.

    Msimu wa 2021/22 ametupia mabao matatu ndani ya ligi kati ya 17 ambayo yamefungwa na timu hiyo baada ya kucheza mechi 15.

    Ameanza kikosi cha kwanza mechi 12 kati ya 15 na alitibua rekodi ya Simba kutofungwa na kupoteza pointi tatu Januari 17,2022 kwa kumtungua Aishi Manula.

    Amewatungua Mbeya Kwanza bao moja dk 44 aliwatungua KMC dk 4 na Simba dk 19 mabao yote alikuwa ndani ya 18 na alitumia mguu wa kulia.

    Mbeya City imekuwa na mwendo mzuri kwa msimu wa 2021/22 na imepoteza mechi mbili kati ya 15 ambazo imecheza.

    Ni mbele ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani,Tanga na ile dhidi ya Namungo iliyochezwa Uwanja wa Ilulu, Lindi.

    Previous articleBARCELONA WAINYOOSHA NAPOLI
    Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA