MWINYI Zahera, Mkurugenzi wa benchi la Ufundi kwa Yanga upande wa Vijana amesema kuwa mchezo wa kesho kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga utakuwa ni mgumu kwa timu zote kulingana na plan, (mpango) wa timu huku akitaja kuwa maandalizi ya kila timu yapo tofauti.
Ameweka wazi kwamba wachezaji wote wa Yanga wanajua kwamba mchezo dhidi ya Mtibwa utakuwa mgumu na hautakuwa rahisi na jana kila mtu anajua kile ambacho kitatokea kuweza kupata pointi tatu.