CHELSEA ni mwendo wa furaha baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Palmeiras kwenye fainali ya Klabu bingwa dunia na kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Romelu Lukaku dakika ya 54 na lile la ushindi lilifungwa na Kai Havertz dakika ya 117 kwa mkwaju wa penalti.
Ni mabao mawili yalipatikana kwa penalti kwa kuwa lile la kusawazisha kwa Palmeiras lilifungwa na Raphael Veiga dakika ya 64 kwa penalti.
Ngoma ilikuwa nzito ambapo Luan Garcia dakika ya 120+6 alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mohamed Bin Zayed.