Ujumbe wa Ali Kamwe kuhusu Juma Kaseja

Mara baada ya Juma Kaseja kufutwa kazi ndani ya kikosi cha Kagera Sugar, Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram:-Katika Maisha ya Ukocha hamna neno kushindwa. Kuna neno Experience. Unaposhinda mechi moja ni Experience nzuri. Ukishinda nyingine kesho ni Experience nzuri zaidi.

“Hivyo hivyo, unapopoteza mechi ni Experience mbaya. Haijalishi ni mechi ngapi utakazofungwa bado inabaki kuwa Experience mbaya zenye utofauti kutokana na wapinzani/ mazingira utakayokutana nayo.

“Kila kinachotokea unapokuwa kwenye Benchi la Ufundi kinakupa uzoefu mpya kila siku kwa ajili ya kujifunza, kuelewa na kuboresha katika mkoba wako.

“Juma Kaseja anabaki kuwa Mmoja wa Makocha bora wa kisasa tulionao hapa Tanzania niliowahi kuwashuhudia wakifundisha mpira.

“Experience aliyoipata Kagera Sugar tangu Championship mpaka Ligi Kuu naamini imemuongezea kitu kwenye safari yake. Amejua kuhusu Football ya Bongo kwa upande wa Ukocha na sio Mchezaji tena

“Kama Kocha, Juma ameshawajua vyema viongozi wa Boli na hesabu za Boli lenyewe la hapa nyumbani. Ameshajua wachezaji wa sasa wako vipi kwenye uwanja wa mazoezi na uwanja wa mechi. Juma ameshapata uzoefu kiasi kuhusu Mashabiki na Vyombo vya Habari vinavyofanya kazi katika nyakati zote za masika na kiangazi.

“Kazi yake ijayo atakuwa na mengi mapya ya kutuonyesha… All The Best Mtaalam wa Mbinu. Hope Siku moja Tutakutana kwenye Benchi la Mpira tukiufanyia kazi mpira wetu,”.