Yanga SC 1-0 Saint George SC Kamwe atoa neno

Wakati ubao wa Uwanja wa Uhuru Septemba 18, 2026 ukisoma  Yanga SC 1-0 Saint George SC, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema kuwa hayo ni maandalizi kwa mechi zinazofuata.

Katika mchezo huo wa kirafiki dakika 45 za awali ngoma ilikuwa 0-0 kwa timu zote uwanjani.

Bao pekee kwa Yanga SC limefungwa na Albert Kangwanda dakika ya 60 ikiwa ni kipindi cha pili zikiwa zimesalia dakika 40 mpira kufika tamati.

Kamwe amesema malengo ni kuona wanakuwa bora jambo ambalo linafanyiwa kazi na benchi la ufundi kwa kila mchezo wanaoshuka uwanjani.

“Malengo ni kuona kwamba tunakuwa imara kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza ipo hivyo na wachezaji wanatambua kila mchezo una ushindani mkubwa,”.

Mchezo ujao kwa Yanga SC ni Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC unatarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2026.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar