MASTAA SENEGAL WAITAKA AFCON

SADIO Mane na Edouard Mendy wamesema kuwa Senegal wamepania kutwaa ubingwa wa Afcon 2021 ili kumpunguzia presha kocha wao Aliou Cisse.

Senegal ambao walifika fainali katika Afcon iliyopita ya 2019 walikuwa miongoni mwa timu zilizopewa nafasi ya kuweza kufika fainali mwanzoni kabisa mwa mashindano haya.

Ilishinda mechi ya kwanza kwa tabu dhidi ya Zimbabwe kisha ikawa kwenye mwendo wa sare mbili mbele ya Guinea na Malawi katika kundi B hali iliyofanya vyombo vya habari kuanza kumkosoa Cisse.

Ubora wa mshambuliaji Mane ambaye anakipiga Liverpool uliweza kuwafanya wakapata ushindi mbele ya Cape Verde, Equatorial Guinea na kutinga hatua ya fainali.

Inakutana na Misri kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa kesho nchini Cameroon ambapo wenyeji hao walitolewa na Misri.