BAKARI Nondo nahodha wa Yanga SC amesema kwa sasa kila mtu ashinde mechi zake ndani ya NBC Premier League kutokana na ushindani uliopo.
Ni Yanga SC hawa ni vinara wakiwa na pointi 60 baada ya mechi 25, kwenye msimamo wanafuatiwa na Simba SC yenye pointi 58 tofauti ya pointi 2.
Timu zote zimecheza mechi 25 zikiwa zimesalia mechi 5 kukamilisha mzunguko wa pili 2025/26 kwenye msako wa bingwa mpya huku Yanga SC wakiwa ni mabingwa watetezi.
Nondo amesema: “Tunatambua ushindani ni mkali na kila timu inapambana kufikia malengo yake. Kikubwa kwa sasa kila mtu ashinde mechi zake ambazo anacheza.
“Tuna mechi ambazo zipo ni ngumu tutapambana kupata matokeo hilo ni jukumu letu wachezaji na tunaomba mashabiki waendelee kuwa nasi nyakati zote,”.
Mchezo ujao kwa Yanga SC ni dhidi ya Mashujaa FC ambapo watakuwa ugenini Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma mwisho wa reli.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.