Orodha ya wachezaji waliotwaa tuzo za Man of the Match mara nyingi

NBC Premier League 2025/26 ina ushindani mkubwa huku ligi ikiwa inakaribia kufika ukingoni kwa bingwa kupatikana.

Ipo wazi kwamba mabingwa watetezi ni Yanga SC wanaongoza ligi wakiwa na pointi 60 nafasi ya pili ni Simba SC ikiwa na pointi 58.

Kila timu imecheza mechi 25 zimesalia mechi 5 kukamilisha mzunguko wa pili wa ligi namba 6 kwa ubora. Kwenye kila mchezo baada ya dakika 90 wadhamini NBC wamekuwa wakitoa tuzo.

Hii hapa rekodi ya wachezaji ambao wametwaa tuzo mara nyingi zaidi namna hii:-

Clatous Chama wa Simba SC huyu ni kiungo anashikilia rekodi ya kuwa kinara kwenye kutwaa tuzo za Man of the Match akiwa nazo 6, anafuatiwa na Feisal Salum wa Azam FC, Kelvin Naftal wa Pamba Jiji FC, Mohamed Salum wa Mtibwa Sugar na Fabrince Ngoy wa Namungo FC hawa wanazo 4.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.